TANGAZA NASI

header ads

"Nikivua Magwanda wote mtakimbia" Tundu Lissu



Makamu mwenyekiti wa Chama cha Drmokrasia na maendeleo Chadema Tundu Lissu mara baada ya kurejea nchini Tanzania,amezungumza na vyombo vya habari.

Miongoni mwa mambo alyozungumza ni pamoja na

"Leo naomba mniruhusu nisiseme mengi sana, nafahamu mmechoka na mimi nimechoka, nimekuwa barabarani toka Jumatano mpaka leo, nchi 4 nilianzia Ujerumani, Uholanzi, Ubelgiji na leo nipo nyumbani, niwatoe hofu tutazungumza mengi yaliyo mema" - @TunduALissu

"Mkiniona nimevaa hivi unaweza usielewe sana kungekuwa na uwezekano wa kuvua magwanda haya, wote mtakimbia kwa sababu huu mwili ukiachia kichwa na uso, huu mwili ni ramani za makovu ya risasi na visu vya Madaktari, huu mwili una vyuma vingi" - @TunduALissu

"Ktk utamaduni wa kawaida watu wanaoponea chupuchupu kama mimi huwa wakikanyaga udongo wa nchi yao huwa wanapiga magoti na kubusu ardhi ya nchi yao, nilitamani na mimi nifanye hivyo, lakini goti halikunji, kwahiyo siwezi tena kupiga magoti" -  @TunduALissu

"Niwape pole wanachama wa @ccm_tanzania kwa kuondokewa na M/Kiti wao wa zamani, huu msiba ni wetu sote, siyo wa Rais @MagufuliJP pekee na kwa sababu ni msiba wetu sote, kesho Mungu akijalia basi tusindikizane tukampe Mkapa heshima yake " - @TunduALissu

"Huu Mguu wa kulia umejaa vyuma kuanzia kwenye Goti hadi kwenye Nyonga, vingine vipo kwenye mkono wa kushoto na Mkono wa kushoto haunyoki, kuna Risasi iko chini ya Mgongo Madaktari walisema ibaki hapo hapo ni salama zaidi kuliko kuitoa" - @TunduALissu

Post a Comment

0 Comments