Na Amiri Kilagalila, Njombe
Edwin Swale aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe,ameshinda kura za maoni katika mkutano mkuu wa jimbo la Lupembe mkoani Njombe kwa kupata kura 138 kati ya kura 421 kuwa mgombea wa ubunge Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM huku Jorum Hongoli aliyekuwa akitetea nafasi yake akipata kura 61.
Edwin Enosy Swale (wakili) alihamia Chama cha Mapinduzi Octoba 2019.
Mkutano wa kura za maoni umefanyika mapema hii Leo katika ukumbi wa Turbo mjini Njombe kwa kuwapigia kura wagombea 19 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
0 Comments