Na Jackline Kuwanda, DODOMA
Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Dodoma
wamejitokeza kumdhamini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika fomu
yake ya kuwania Urais.
Akizungumza na waandishi wa habari Dayana Moses
Mwalukwa ambaye ni katibu wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Dodoma
mjini amesema wanawake elfu moja (1000) wamejitokeza kumdhamini Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya
wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Joyce George amesema kwa upande wa wakina
mama amewasaidia kwa kiasi kikubwa hasa katika upatikanaji wa mikopo huku Joyna
Godilisious Makewa ambaye ni mwanachama wa chama hicho akisema kuwa na ni
kada wa UWT akisema amejitokeza kumdhami Rais kwasababu amefanya mambo mengi
ikiwemo katika sekta ya Elimu.
June 17 ,2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alichukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais kwa
tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM kwenye Makao Makuu ya Chama hicho jijini
Dodoma ambapo alikabidhiwa fomu hizo na Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt Bashiru
Ally.
0 Comments