TANGAZA NASI

header ads

Mafuriko mto Ruvu yaathiri mashamba ya Chauru



Na Omary Mngindo, Ruvu
Mei 5

MVUA zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini, kwa kiasi kikubwa imeathiri mashamba eka 871 yaliyopo katika Ushirika wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU).

Mashamba hayo yaliyoko katika Kijiji cha Visezi, Kata ya Vigwaza halmashairi ya Chalinze Baganoyo Pwani, mbali ya kuwaathiri wanachama 430, pia imewakosesha ajira za kutwa wakazi 600 wanaotoka maeneo mbalimbali wanaong'olea mpunga, wakiwemo waendesha pikipiki wanaobeba mbolea na kusafirisha wakulima.

Hayo yameelezwa na Wallwa Makoye Ofisa Ugani wa ushirika, akizungumza na waandishi wa habari kwenye mashamba hayo, huku akiitaja mifereji iliyoathirika ni namba 5 eka 187, namba 7 eka 171, namba 8 eka 212, namba 6 eka 161 wakati namba 4 eka 140.

Makoye alisema kuwa changamoto hiyo imekuwa kubwa kwa wanachama hao, ambao kwa msimu huu wengine wamelazimika kupanda mbegu zaidi ya mara tatu, huku wengine wakikata tamaa kutokana na mafuriko hayo ambayo yamefunika mashamba kadhaa.

"Ushirika wetu una mashamba ekta 1,800, kati ya hizo eka 871 wanachama wetu 430 wameshindwa kupanda kutokana na athari ya mvua, ambayo imeathiri baadhi ya maeneo ya mashamba yetu, kama mnavyojionea hali ni mbaya kwelikweli," alisema Makoye.

Nae Ofisa Umwagiliaji Peter Mbembela alisema kuwa hali ya mafuriko yaliyopo kwenye mashamba hayo yamesababisha kutopandwa, huku akieleza kuwa kukosekana kwa mashine ya kutolea maji inachangia kuwepo kwa hali hiyo.

Meneja wa Ushirika huo Victoria Olotu amelalamikia tabia ya baadhi ya jamii ya wafugaji kupitisha mifugo yao kwenye mashamba, hali inayosababisha ubaribifu wa mazao, ikiwemo vitalu, mashamba ya mahindi na viazi huku akiiomba Serikali kuwaongezea nguvu ya kudhibiti vitendo hivyo.

"Mbali ya mafuriko jambo lingine linalotuathiri ni hali ya mifugo inayoingizwa na baadhi ya wafugaji, ambapo wanaharibu mazao mbalimbi ikiwemo vitalu vya mpunga vinavyoanfaliwa na wanachama wetu, tunaiomba Serikali itusaidie katika hili," alisema Olotu.

Mkulima Fatiha Haji alisema kwamba alipanda mara ya kwanza maaji yakaingi na kuharibu mbegu, akarudia mara ya pili hali ikahirudia sasa anatafuta mbugu ili apande tena, hali in atoms a babushka hasara kubwa, huku akiiomba Serikali kupitia Wizara kuwapatia msaada.

Sadala Chacha Mwenyekiti wa CHAURU alisema kuwa kilimo hicho cha msimu wa 2019/2020, mashamba yote ekta 1800 yalishalimwa na kipandikizwa mbegu, lakini kuyokana na mvua yameathiri mashamba hayo, hivyo wakulima 350 bado hawajapandikiza.

"Msimu huu tunakabiliwa na changamoto kubwa katika kufanikosha kilimo kwenye ushirika wetu, wanachama wamefuata taratibu zote za kilimo sanjali na kupanda, lakini maji yamevamia kwenye mashamba kama mlivyojionea," alimalizia Sadala.

Post a Comment

0 Comments