Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Baada ya Serikali kutangaza kufungua vyuo vyote na shule kwa kidato cha
sita bodi ya mikopo ya elimu ya juu imetoa kiasi cha sh bilioni 63. 83
kwa ajili ya awamu ya tatu ya wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 29, 2020 Mkurugenzi wa Bodi
ya mikopo Abdul Razaq Badru amesema fedha hizo ni kwa ajili ya awamu ya
tatu ambao awamu mbili za mwanzo tayari zilishatolewa.
"Sisi kama bodi ya mikopo tayari tumeshatoa fedha kwa ajili ya mikopo
kiasi Cha shilingi bil.63.83, ikiwa ni awamu ya tatu baada ya awamu ya
pili kukamilika" amesema Badru.
Amesema tayari fedha hizo zimeshapelekwa katika vyuo vyote vyenye sifa
na tayari maafisa mikopo wamesha pelekwa vyuoni kwa ajili ya
kushughilikia na mikopo ya kuhakikisha wanafunzi wanapata kwa wakati.
Amesema wanafunzi wasiogope warudi vyuoni kuendelea na masomo kwa sababu
serikali imejipanga kwa kila kitu na kuwataka kuanza kuripoti kwa ajili
ya kujisajili.
"Naomba wanafunzi wasiogope warudi shuleni ili kuendelea na masomo kwa ajili ya kuendelea na masomo, " amesema.
Amebainisha kuwa usajili umeanza leo utaendelea hadi Jumapili lakini watakaochelewa usajili utaendelea Jumatatu.
Amesema wanafunzi waliopo 132, 119 na taasisi zilizopelekewa fedha hadi sasa ni zaidi ya 70 zilizopo hapa nchini.
Amesema malipo ni ya siku 60 ambapo ni kwa ajili ya malazi na chakula ambayo wanafunzi wanaita bumu.
0 Comments