TANGAZA NASI

header ads

Ujerumani kupanua onyo la kutosafiri hadi katikati mwa mwezi Juni

 
Marekani leo imerekodi kesi zaidi ya milioni moja za maambukizi ya virusi vya corona huku vifo vikipindukia 58,000 na kuzidi idadi ya Wamarekani waliouawa katika vita ya Vietnam.
Rais Donald Trump amesema utawala wake unazingatia kufanya ukaguzi wa virusi kwenye baadhi ya ndege za kimataifa ili kukomesha kuenea kwa maambukizi.


Nchini Ujerumani, baraza la mawaziri limeidhinisha kupanuliwa kwa onyo la kuzuia safari za kitalii nje ya nchi.

Wakati huo Ujerumani imerekodi visa 1,304 zaidi vya COVID-19 huku idadi ya vifo mpaka sasa ni 6,115, kulingana na taasisi ya Robert Koch.

Brazil imetangaza vifo zaidi ya 5,000 huku Ufaransa ikisema italegeza vizuizi endapo kiwango cha maambukizi kitabaki chini ya 3000 kwa siku.

 Uturuki imeendelea kuzifunga shule hadi mwishoni mwa mwezi ujao. Na visa vya maambuki nchini Urusi vinakaribia 100,000.

Post a Comment

0 Comments