Nahodha wa Tanzania anae kipiga kunako klabu ya Aston Villa ya Uingereza amesema njia bora ya vilabu kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ni kuboresha ligi ya ndani kwanza.

Ikumbukwe kabla ya Samatta kwenda kucheza soka la kulipwa nje alikuwa akikipiga ndani ya Klabu ya Simba kisha TP Mazembe, KRC Genk na hatimaye Aston Villa.

“Ni dhahiri kwamba katika ligi yetu, ni timu chache tu zina uwezo wa kujenga kikosi cha ushindani ambacho kinaweza kuleta athari chanya katika ligi ya mabingwa ya CAF (CAF CL) na Kombe la Shirikisho la CAF,” amesema.

“Kwa kuzingatia hii, timu zetu ambazo zinafanikiwa kucheza katika mashindano makubwa kwenye bara huwa zinafanya vizuri katika hatua za awali kwa sababu zinakutana na timu ambazo ni za kiwango sawa na wao na wakati mashindano yanaendelea, mchezo unakua mgumu kwa sababu wanaanza kukutana na timu za viwango vya juu “alisema nahodha waTaifa Stars na mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta